top of page

"Let's Build Your Success Story"📌

  • Writer: Joseph Magweiga Marwa
    Joseph Magweiga Marwa
  • Jul 9, 2023
  • 4 min read

Updated: Jul 10, 2023


Tumetumia makala hii kukupa maarifa na ufafanuzi, wa huduma ambazo tunajua kwa uhakika zitakusadia kwa namna moja au nyingine. Maalum kwa wakurugenzi na wasimamizi wa miradi.


Katika safari ya mafanikio ya biashara yako jambo la muhimu ni maono au malengo ya wapi unataka kufika. Kisha wazo la biashara litakalokupa matokeo na kufanya ufikie malengo na kutimiza maono yako.


Jambo lingine la muhimu sana kwa sasa ni aina ya watu wa kusafiri nao kwenye bus la maono yako ili ufikie ndoto zako. Hauna haja ya kuwaacha watu ambao siyo sahihi kukalia siti wakati wanapoteza muda na hakuna wanachoongeza kwenye miradi yako.


Kwa kujua kuwa mafanikio katika biashara yanaletwa na watu sahihi na mikakati bora (right people and better strategies). Pamoja na team nzuri uliyo nayo sasa au unayotaka kuanza nayo, unaweza kutukaribisha tukawa sehemu ya team yako, kwa sababu tunao uzoefu, maarifa, ubobezi na ufahamu wa kutosha wa soko na aina ya biashara unayoendesha tunaweza kuleta mapinduzi ukitupa siti kwenye bus hilo.


Hebu tusikuchoshe sana unaweza kuchagua namba ya maeneo ambayo ungependa kupata usaidizi na tunaweza kukusaidia kwa weledi na haraka pengine kwa wakati kuliko matazamio yako. Fuatana nasi kwa ufupi, utaelewa tunamaanisha nini.


Tuanze na Muundo wa biashara (Business Structure). Huenda unataka kuanza kwa usajili wa kampuni au jina la biashara au kubadilisha muundo ulionao kwenda mwingine.


Tofauti ya kampuni na jina la biashara ni muundo wa uendeshaji tu. Kampuni itahitaji mtu zaidi ya mmoja (kuanzia 2) na kuwa na wakurugenzi. Kwa ufupi itakuwa taasisi na inajitemea katika uendeshaji. Kwa biashara ya mikopo kuna ukomo wa idadi ya wateja ambayo ni 100 au mzunguko wa Mil.200 zaidi ya hapo lazima uhamie kwenye mfumo wa kampuni.


Jina la biashara unaweza kutumia kama mtu binafsi (sole proprietorship au mkopeshaji binafsi au kama partnership mkiungana na watu kuanzia 2 na wasiozidi 20 hivi).


Endapo unapenda kuaminika na kutoa huduma kwa taasisi kubwa kampuni ni mahali sahihi. Lakini kama hautaki mlolongo na utitili wa kodi na unataka mahali pa kuanzia basi jina la biashara tu linatosha (Lakini suala la kuaminika ni changamoto) maana huitwa biashara ya mtu mmoja, akiugua inaugua, akisafiri inasafiri, akifariki inafariki. Kazi ni kwako kuchagua muundo sahihi


DOCUMENTS MUHIMU KWA BIASHARA YAKO AMBAZO USIPOKUWA NAZO NI SAWA NA UPOFU😇


Baada ya kuchagua muundo wa biashara kinachofuata ni documents za muhimu za kukusaidia kuendesha biashara hiyo au kuombea mkopo au uwekezaji kwa wawekezaji au watu wanaotaka uwazungushie hela zao kwenye mradi au biashara yako.


1. Business Plan - Mpango kazi au mchanganuo wa biashara. Hii ndiyo ramani ya biashara yako na inatoa maelezo yote ya muhimu, dira na maono pamoja na mikakati yako.


Hueleza juu ya bidhaa au huduma unazotoa, inajibu maswali kama wateja wako ni wakina nani? wako wapi? na utawafikiaje? (kipande cha marketing plan au mpango masoko na namna ya kusambaza bidhaa au hiduma zako)

Kisha itaelezea alama za muhimu (mile stones) za kuchukua hadi kufikia malengo. Inaeleza pia juu ya fedha, bajeti na mipango (financial plan) kwa miaka kadhaa (3 hadi 5) hivyo hauna haja ya kuwaza badala yake kufanya marekebisho kila muda ili iendane na uhalisia.


2. Company Profile - Wasifu wa kampuni. Kwa wanaoomba tenda kwenye taasisi mbalimbali lazima uwe nayo ili wajue vizuri anayewahudimia na team yake wana uwezo kiasi gani.


3. Strategic Plan - Hii itaeleza juu ya mikakati ya kampuni kati ya miaka 3 hadi 5 (Muhimu sana)


4. Budget Plan - Hii ni bajeti ambayo ni muhimu ili kufikia malengo. Inaweka malengo ya makusanyo (Mapato), utumie kiasi gani ili usizidishe ukaingia hasara pia juu ya manunuzi na matumizi mengineyo. Kwa ufupi usipokuwa nayo ni kuiambia hela uliyoipata kwa shida ipotee bila mipango


5. Audit Plan - Mpango wa ukaguzi. Ni muhimu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara juu miradi yako na kuona mapungufu kabla kukwama. Ukaguzi huu unaweza kulenga kupima ufanisi, matumizi ya rasilimali ikilinganishwa na matokeo unayoyapata, mifumo inayotumika na vitabu vya mahesabu vyote


6. Management Accounts - Itapima biashara na mwenendo wake kwa miezi inayofuata baada ya mwaka wa mahesabu kuisha.


7. Cash-flow projections - Mtiririko wa fedha zinazoingia na kutoka kwenye miradi na biashara zako zote. Endapo mradi unatumia zaidi ya vile unavyoingiza basi ni dalili mbaya kwamba haukusanyi fedha za kutosha kuendeshea mradi wako.


8. Company policy au Lending Policy kwa Microfinance - Biashara nyingi za leseni za daraja "A", zile zinazotolewa na Brela chini ya wizara ya viwanda na biashara zinahitajika kwa muendeshaji bila kujali ni kampuni au mtu mmoja.


9. Mikataba ya makubaliano na Fomu za maombi - Ni vizuri kujenga utamaduni wa kuendesha taasisi au biashara kwa makubaliano yaliyo kwenye karatasi na siyo maneno tu. Hivyo ni muhimu kuwa na mikataba kulingana na huduma unayotoa.


Pamoja na hayo yaliyotangulia tunaweza kutoa usaidizi kwenye team au taasisi yako katika vitu vifuatavyo:


A. Leseni (inategemeana inatolewa na mamlaka gani)

B. Vibali vya makato hazina siku 30 hadi 45

C. Utatuzi wa changamoto za kikodi na mahesabu ya kampuni yako

D. Statutory payments na filing kama NSSF, WCF, TASIWU, SDL, PAYE, VAT, BRELA, BOT

E. Financial Reports (zote)

F. Business Set-Up kwa miradi yote

G. Kufungua au kufunga bila kuacha madeni

H. Katiba na malengo ( kampuni, vikundi na saccos).


Cha kufanya endapo utahitaji ufafanuzi au huduma piga☎️ +255 747 912 965 au WhatsApp No. 0759 551 592 sasa hivi upate huduma.


Kasi, ubora na uaminifu wetu utakushangaza

Hauna haja ya kulipia kazi yote kabla ya kuipokea. Utapewa mkataba wa kukulinda (mkataba wa makubaliano) kisha utalipia 30% ya thamani ya mkataba na kazi itaanza mara moja.


Tupo jengo la Mwenge Tower, inayotazamana na Mlimani City au tembelea www.zatra.co


Wako,


Joseph Marwa

Director | Zatra


CPA. Alto Mwangoa

Director | Zatra


CPA. Michael Mtoi

CFO | Zatra

 
 
 

Comments


bottom of page